Uchunguzi wa Hali ya Mtoto: Miezi 2
Kwenye uchunguzi wa miezi 2, mtoa huduma wa afya atamchunguza mtoto na kuuliza jinsi mambo yanavyoendelea nyumbani. Fomu hii inaelezea baadhi ya kile unachoweza kutarajia.
Ukuaji na uwezo
Mtoa huduma wa afya atauliza maswali kuhusu mtoto wako. Atamwangalia mtoto wako ili kupata habari kuhusu ukuaji wake. Kwa ziara hii, kuna uwezekano mtoto wako anafanya baadhi ya yafuatayo:
-
Kutabasamu kwa kusudi, kama vile kumjibu mtu mwingine (huitwa “tabasamu ya jamii”)
-
Kugonga au kusukuma vitu vilivyo karibu
-
Kukufuatiliza kwa macho yake unapotembea chumbani
-
Kuanza kuinua au kudhibiti kichwa chake
Vidokezo vya kulisha
Endelea kumpa mtoto wako maziwa ya mama au fomula. Ili kumsaidia mtoto wako ale vizuri:
-
Wakati wa mchana, mlishe angalau kila baada ya saa 2 hadi 3. Huenda ukahitajika kumwamsha mtoto kwa mlo wa mchana.
-
Usiku, mlishe mtoto anapoamka, mara nyingi kila baada ya saa 3 hadi 4. Ni Sawa mtoto akilala kwa muda mrefu kuliko huu. Huenda usihitaji kumwamsha mtoto kwa milo ya usiku.
-
Vipindi vya kunyonyesha vinapaswa kudumu takribani dakika 10 hadi 15 . Ukitumia chupa, mpe mtoto wako aunsi 4 hadi 6 (mililita 118 hadi 177) za maziwa ya mama au fomula.
-
Ikiwa una wasiwasi kuhusu kiasi au mara ambazo mtoto wako anakula, mwambie mtoa huduma wa afya.
-
Mwulize mtoa huduma wa afya ikiwa mtoto wako anapaswa kupata vitamini D.
-
Usimpe mtoto wako chochote kula mbali na maziwa ya mama au fomula. Mtoto wako ni mchanga sana kuweza kula vyakula vigumu au vioevu vingine. Mtoto mchanga hapaswi kupewa maji matupu.
-
Fahamu kwamba watoto wengi walio na umri wa miezi 2 hutema baada ya kula. Mara nyingi hii ni hali ya kawaida. Wasiliana na mtoa huduma mara moja mtoto akitema mara kwa mara kwa nguvu, au akitema chochote ambacho si maziwa wala fomula.
Vidokezo vya usafi
-
Watoto wengine huenda haja kubwa (choo) mara chache kwa siku. Wengine huenda haja mara moja kila baada ya siku 2 hadi 3 . Chochote kinachohusiana na hili ni kawaida.
-
Ni sawa ikiwa mtoto wako anaenda haja kubwa mara chache kuliko kila baada ya siku 2 hadi 3 ikiwa mtoto ana afya nzuri. Lakini ikiwa mtoto anasumbuka, anatema zaidi ya kawaida, anakula kidogo kuliko kawaida, au ana choo kigumu sana, mwambie mtoa huduma wa afya. Huenda mtoto hapati choo (ameshindwa kuenda haja kubwa).
-
Choo kinaweza kuwa cha rangi ya manjano hadi hudhurungi hadi kijani. Ikiwa ni cha rangi nyingine, mwambie mtoa huduma wa afya.
-
Mwogeshe mtoto wako mara chache kwa wiki. Unaweza kumwogesha mara kwa mara ikiwa mtoto anafurahia. Lakini kwa sababu unasafisha mtoto wakati wa kubadilisha nepi, huhitaji kumwogesha kila siku.
-
Ni Sawa kutumia krimu kidogo au losheni kwenye ngozi ya mtoto. Usiweke losheni kwenye mikono ya mtoto.
Vidokezo vya kulala
Katika umri wa miezi 2, watoto wengi hulala kwa takribani saa 15 hadi 18 kila siku. Ni kawaida kwa watoto kulala kwa muda mfupi siku nzima, badala ya saa kwa wakati. Huenda mtoto akawa anahangaika kabla ya kuenda kulala usiku takribani saa 6 jioni hadi saa 9 usiku. Hii ni hali ya kawaida. Ili kumsaidia mtoto wako kulala salama na vizuri:
-
Mweke mtoto mchanga alale kwa mgongo wake kwa usingizi kidogo na kulala hadi afikishe mwaka 1. Hii inaweza kupunguza hatari ya SIDS, mpumuo na kusakamwa. Usiwahi kumlaza mtoto upande wake wala kwa tumbo kwa usingizi mrefu au mfupi. Ikiwa mtoto ameamka, mpe muda alale kwa tumbo mradi tu uwe unamwangalia. Hii husaidia mtoto kuwa na misuli thabiti ya tumbo na shingo. Pia hii itasaidia kupunguza kichwa cha mtoto wako kuwa bapa. Tatizo hili linaweza kutokea wakati watoto wanatumia muda mwingi kulala kwa migongo yao.
-
Mwulize mtoa huduma wa afya ikiwa unapaswa kumruhusu mtoto wako kulala na titibandia. Kulala na titibandia kumeonyesha kupunguza hatari ya SIDS. Lakini usimpe hadi baada ya kukamilisha kunyonya. Ikiwa mtoto wako hataki titibandia, usijaribu kumlazimisha atumie.
-
Usiweke hori, mto, mablanketi yaliyolegea, au wanyama bandia katika hori. Vitu hivi vinaweza kumkosesha mtoto hewa.
-
Kumfunga mtoto kunamaanisha kumfungia mtoto wako aliyezaliwa kwenye blanketi, lakini na nafasi ya kutosha ili aweze kusogeza nyonga na miguu yake. Kumfungia mtoto kwenye blanketi kunaweza kusaidia mtoto wako kuhisi salama na kulala. Unaweza kununua blanketi maalum la kumfungia lililotengenezwa ili kurahisisha kufungia. Lakini usitumie blanketi la kumfungia ikiwa mtoto wako ana umri wa miezi 2 au zaidi, au ikiwa mtoto anaweza kubingiria mwenyewe. Kumfungia kwenye blanketi kunaweza kuongeza hatari ya SIDS (dalili za kifo cha ghafla cha mtoto mchanga) ikiwa mtoto aliyefungiwa kwenye blanketi atabingirika kwenye tumbo lake. Miguu ya mtoto wako inapaswa kuweza kusonga juu na nje kwenye nyonga. Usiweke miguu ya mtoto wako ili ishikane na kunyoka kuelekea chini. Hali hii huongeza hatari hivi kwamba viungo vya nyonga havitakua na kuimarika inavyofaa. Hali hii inaweza kusababisha tatizo linaloitwa displezia na kutengana kwa nyonga. Pia kuwa makini kuhusu kumfungia mtoto kwenye blanketi ikiwa hali ya hewa ni yenye joto. Kutumia blanketi zito katika hali ya hewa yenye joto kunaweza kumfanya mtoto wako kuwa na joto kupita kiasi. Badala yake tumia blanketi jepesi au shuka kumfungia mtoto.
-
Usimweke mtoto wako kwenye kochi wala kiti cha mikono ili kulala. Kulala kwenye kochi au kiti cha mikono humweka mtoto kwenye hatari zaidi ya kifo, ikiwemo SIDS.
-
Usitumie viti vya mtoto mchanga, viti vya gari, vitembezi, keria za watoto wachanga au bembea za mtoto mchanga kwa kulala mara kwa mara na usingizi kidogo wa kila siku. Hatua hizi zinaweza kusababisha uzuiaji wa njia ya hewa au mtoto kukosa hewa.
-
Ni Sawa kumlaza mtoto akiwa hajalala. Pia ni Sawa kumwacha mtoto alie akiwa kitandani, lakini kwa dakika chache tu. Katika umri huu, watoto hawako tayari “kulia wenyewe hadi walale.”
-
Ikiwa unatatizika mtoto wako kulala, mwulize mtoa huduma wa afya vidokezo.
-
Usishiriki kitanda (kulala pamoja) na mtoto wako. Kulala kwenye kitanda kimoja kumeonyesha kuongeza hatari ya SIDS. American Academy of Pediatrics (AAP) inapendekeza kuwa watoto wachanga walale kwenye chumba kimoja na wazazi wao. Wanapaswa kuwa karibu na kitanda cha wazazi wao, lakini katika kitanda tofauti au hori bora. Mpangilio huu wa kulala unapaswa kufanywa kwa mwaka wa kwanza wa mtoto, ikiwezekana. Lakini unapaswa kufanya hivyo kwa angalau miezi 6 ya kwanza.
-
Weka hori, matenga ya watoto na yadi za kucheza katika maeneo yasiyo na hatari. Hii inamaanisha kusiwe na kamba, nyaya, au mapazia ya dirisha yanayoning`inia. Hii itapunguza hali ya kujinyonga.
-
Usitumie mapigo ya moyo ya mtoto na monita au vifaa maalum kusaidia kupunguza hatari ya SIDS. Vifaa hivi vinajumuisha kabari, vishikaji nafasi na magodoro maalum. Vifaa hivi havijathibitisha kuzuia SIDS. Vimesababisha kifo cha mtoto mchanga kwa nadra sana.
-
Zungumza na mtoa huduma wa afya wa mtoto wako kuhusu masuala haya na mengine ya afya na usalama.
Vidokezo vya usalama
-
Ili kuzuia michomo, usibebe wala kunywea vioevu moto kama vile kahawa karibu na mtoto. Punguza halijoto ya kichemshio cha maji hadi 120.0°F (49.0°C) au chini.
-
Usivute wala kuruhusu wengine wavute sigara karibu na mtoto. Ikiwa wewe au wanafamilia wengine wanavuta sigara, vutia nje ukiwa umevaa jaketi na kisha uvue jaketi kabla ya kumshika mtoto. Usiwahi kuvuta sigara karibu na mtoto.
-
Ni sawa kumpeleka mtoto nje. Lakini kaa mbali na maeneo yeliyobanana na kujaa watu ambapo viini vinaweza kusambaa.
-
Unapompeleka mtoto nje, usikae muda mrefu sana kwenye mwangaza wa jua wa moja kwa moja. Mfunike mtoto au nenda kwenye kivuili.
-
Mweke mtoto kwenye kiti cha gari kinachoangalia nyuma ukiwa garini kila mara. Hii inapaswa kuwekwa kwenye kiti cha nyuma kulingana na maelekezo ya kiti cha gari. Usiwahi kumwacha mtoto peke yake garini.
-
Usimwache mtoto wako kwenye sehemu ya juu, kama vile meza, kitanda wala kochi. Anaweza kuanguka na kuumia. Pia, usimweke mtoto kwenye kiti kinachorusha kwenye sehemu ya juu.
-
Huenda ndugu wakubwa wakataka kumshika, kucheza naye na kutaka kumjua mtoto.
-
Wasiliana na mtoa huduma wa afya mara moja ikiwa mtoto wako ana umri chini ya miezi 3 na ana homa (tazama Homa na watoto, hapa chini).
Homa na watoto
Tumia kipimajoto cha dijitali kila mara kuangalia halijoto ya mtoto wako. Usiwahi kutumia kipimajoto cha zebaki.
Kwa watoto wachanga na wanaodema, hakikisha kuwa umetumia kipimajoto cha rektamu inavyofaa. Kipimajoto cha rektamu kinaweza kutoboa shimo kwa bahati mbaya katika rektamu. Pia kinaweza kusambaza viini kutoka kwenye choo. Fuata maelekezo ya mtengenezaji bidhaa kwa matumizi sahihi kila mara. Ikiwa huhisi vizuri kupima halijoto ya rektamu, tumia mbinu nyingine. Unapozungumza na mtoa huduma wa afya wa mtoto wako, mwambie mbinu uliyotumia kupima halijoto ya mtoto wako.
Hii hapa miongozo ya halijoto ya homa. Halijoto za sikio ni sahihi baada ya umri wa miezi 6. Usipime halijoto ya kinywani hadi mtoto wako afikishe angalau miaka 4.
Mtoto chini ya miezi 3:
-
Mwulize mtoa huduma wa mtoto wako jinsi unavyopaswa kupima haijoto.
-
Halijoto ya rektamu au paji la uso (ateri ya panja) ya 100.4°F (38°C) au juu zaidi, au kama ilivyoagizwa na mtoa huduma
-
Halijoto ya kwapa ya 99°F (37.2°C) au juu zaidi, au ilivyoagizwa na mtoa huduma
Chanjo
Kulingana na mapendekezo kutoka CDC, kwenye ziara hii mtoto wako anaweza kupata chanjo zifuatazo:
Chanjo husaidia kudumisha afya ya mtoto wako
Chanjo husaidia mwili wa mtoto wako kuunda kinga dhidi ya magonjwa mabaya. Kumpa mtoto wako chanjo zote pia kutasaidia kupunguza hatari SIDS kwa mtoto wako. Nyingi hutolewa kwa mfuatano wa dozi. Ili kujikinga, mtoto wako anahitaji kila dozi wakati unaofaa. Chanjo nyingi za mseto zinapatikana. Zinaweza kusaidia kupunguza idadi ya sindano zinazohitajika ili kumchanja mtoto wako dhidi ya magonjwa haya yote muhimu. Zungumza na mtoa huduma wa afya wa mtoto wako kuhusu manufaa ya chanjo na hatari yoyote zinazoweza kuwa nazo. Pia uliza cha kufanya ikiwa mtoto wako atakosa kupata dozi. Hali hii ikitokea, mtoto wako atahitaji chanjo za ufuatiliaji ili akingwe kikamilifu. Baada ya kupewa chanjo, watoto wengine wana madhara madogo kama vile wekundu na kuvimba pale walipodungwa sindano ya chanjo, homa, kuhangaika au kukosa usingizi. Zungumza na mtoa huduma kuhusu jinsi ya kudhibiti hali hizi.
Uchunguzi unaofuata kwenye: _______________________________
MADOKEZO YA MZAZI: