Health Encyclopedia
A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z A-Z Listings

Uchunguzi wa Hali ya Mtoto: Mtoto Aliyezaliwa

Uchunguzi wa kwanza wa mtoto wako unaweza kutendeka ndani ya wiki moja baada ya kuzaliwa. Kwenye ziara hii ya mtoto aliyezaliwa, mtoa huduma wa afya atamchunguza mtoto wako na kuuliza maswali kuhusu siku chache za kwanza nyumbani. Fomu hii inaelezea baadhi ya kile unachoweza kutarajia.

Homa ya Nyongo ya Manjano

Watoto wote huwa na umanjano kwenye ngozi na sehemu nyeupe ya macho (homa ya nyongo ya manjano) wiki ya kwanza ya maisha. Mtoa hudumaw wako wa afya atakushauri ikiwa unahitaji kiwango cha bilirubini ya mtoto wako kichunguzwe. Mtoa huduma wako atakushauri ikiwa mtoto wako anahitaji uchunguzi wa ufuatiliaji au anahitaji matibabu ya picha.

Ukuaji na uwezo

Mtoa huduma wa afya atauliza maswali kuhusu mtoto wako aliyezaliwa. Atamwangalia mtoto wako ili kupata habari kuhusu ukuaji wake. Kwa ziara hii, kuna uwezekano mtoto wako aliyezaliwa anafanya baadhi ya yafuatayo:

  • Kupepesa macho kwenye mwangaza mwingi
  • Kujaribu kuinua kichwa chake
  • Kugaagaa na kunyonganyonga mwili. Kila mkono na mguu unapaswa kusonga takribani hatua sawa. Ikiwa mtoto anapendelea upande mmoja, mwambie mtoa huduma wa afya.
  • Kushtuka anaposikia kelele

Vidokezo vya kulisha

Mother holding newborn baby

Ni kawaida kwa mtoto aliyezaliwa kupoteza hadi asilimia 10 ya uzito wake wa kuzaliwa wiki ya kwanza. Uzito huu hurejea akiwa na takribani umri wa wiki 2. Ikiwa una wasiwasi kuhusu uzito wa mtoto wako aliyezaliwa, mwambie mtoa huduma wa afya. Ili kumsaidia mtoto wako ale vizuri, fuata vidokezo hivi:

  • Maziwa ya mama yanapendekezwa kwa miezi 6 ya kwanza ya mtoto wako.
  • Mtoto wako anapaswa kutokunywa maji isipokuwa mtoa huduma wake wa afya apendekeze hivyo.
  • Wakati wa mchana, mlishe angalau kila baada ya saa 2 hadi 3. Huenda ukahitaji kumwamsha mtoto wako kwa mlo wa mchana.
  • Usiku, mlishe mtoto kila baada ya saa 3 hadi 4. Kwanza, mwamshe mtoto wako ili kumlisha ikihitajika. Pindi mtoto wako aliyezaliwa anaporejesha uzito wake, unaweza kuchagua kumruhusu alale hadi ahisi njaa. Jadili hili na mtoa huduma wa afya wa mtoto wako.
  • Mwulize mtoa huduma wa afya ikiwa mtoto wako anapaswa kupata vitamini D.

Ukimnyonyesha

  • Pindi maziwa yako yanapokuja, unapaswa kuhisi matiti yako yakiwa yamejaa kabla ya kumlisha na laini na yaliyofungua baadaye. Hali hii inaweza kumaanisha kuwa mtoto wako anapata chakula cha kutosha.
  • Vipindi vya kunyonyesha kwa kawaida huchukua dakika 15 hadi 20. Ukimnyonyesha mtoto maziwa ya mama kutoka kwenye chupa, mpe aunsi 1 hadi 3 (mililita 30 hadi 89) kwa unaponyonyesha.
  • Watoto wanaonyonyeshwa huenda wakataka kula mara kwa mara zaidi ya saa 2 hadi 3. Ni Sawa kumlisha mtoto wako mara kwa mara ikiwa anaonekana ana njaa. Zungumza na mtoa huduma wa afya ikiwa una wasiwasi kuhusu tabia za kunyonya au ongezeko la uzito wa mtoto wako.
  • Huenda ikachukua muda fulani kujua kunyonyesha. Huenda ukahisi vibaya mara ya kwanza. Ikiwa una maswali au unahitaji usaidizi, mshauri wa unyonyeshaji anaweza kukupa vidokezo.

Ikiwa unatumia fomula

  • Tumia fomula iliyotengenezwa kwa ajili ya wattoo wachanga tu. Ikiwa unahitaji usaidizi kuchagua, mwulize mtoa huduma wa afya pendekezo. Maziwa ya ng`ombe ya mara kwa mara si chakula bora kwa mtoto aliyezaliwa.
  • Mlishe karibu aunsi 1 hadi 3 (mililita 30 hadi 89) za fomula kila mlo.

Vidokezo vya usafi

  • Watoto wengine waliozaliwa huenda haja kubwa (choo) baada ya kila mlo. Wengine huenda haja mara chache. Yote ni kawaida. Badilisha nepi kila inapokuwa na unyevu au chafu.
  • Ni kawaida kwa choo cha mtoto aliyezaliwa kuwa manjano, majimaji na kufanana na kama kilicho na mbegu ndogo. Rangi inaweza kuwa kuanzia manjano hadi manjano hafifu hadi kijani. Ikiwa ni cha rangi nyingine, mwambie mtoa huduma wa afya.
  • Mvulana anapaswa kuwa na mtiririko imara anapoenda haja ndogo. Ikiwa mwanao hana, mwambie mtoa huduma wa afya.
  • Mwogeshe mtoto wako kwa sifongo hadi kitovu kitakapodondoka. Ikiwa una maswali yoyote kuhusu kutunza kitovu, mwulize mtoa huduma wa afya wa mtoto.
  • Fuata mapendekezo ya mtoa huduma wako wa afya kuhusu jinsi ya kutunza kitovu. Utunzaji huu unaweza kujumuisha:
    • Kudumisha usafi wa eneo na kulikausha
    • Kukunja sehemu ya juu ya nepi ili hewa ifikie kitovu
    • Kusafisha kitovu taratibu kwa kitambaa cha mtoto au kwa pamba iliyowekwa kwenye alkoholi ya kusugua
  • Wasiliana na mtoto huduma wako wa afya ikiwa eneo la kitovu lina usaha au wekundu.
  • Baada ya kitovu kudondoka, mwogeshe mtoto wako mara chache kwa wiki. Unaweza kumwogesha mara kwa mara ikiwa mtoto anafurahia. Lakini kwa sababu unasafisha mtoto wakati wa kubadilisha nepi, huhitaji kumwogesha kila siku.
  • Ni Sawa kutumia krimu kidogo au losheni kwenye ngozi ya mtoto. Usiweke losheni kwenye mikono ya mtoto.

Vidokezo vya kulala

Watoto waliozaliwa kwa kawaida hulala takribani saa 18 hadi 20 kila siku. Ili kumsaidia mtoto wako kulala salama na vizuri na kuzuia SIDS (dalili za kifo cha ghafla cha mtoto mchanga):

  • Mweke mtoto mchanga alale kwa mgongo wake kwa kipindi kizima cha kulala hadi afikishe mwaka 1. Hii inaweza kupunguza hatari ya SIDS, mpumuo na kusakamwa. Usiwahi kumlaza mtoto upande wake wala kwa tumbo kwa usingizi mrefu au mfupi. Ikiwa mtoto ameamka, mpe muda alale kwa tumbo mradi tu uwe unamwangalia. Hii husaidia mtoto kuwa na misuli thabiti ya tumbo na shingo. Pia hii itasaidia kupunguza kichwa kuwa bapa jambo linaloweza kutokea wakati watoto wanatumia muda mwingi kulala kwa migongo yao.
  • Mpe mtoto titibandia kwa ajili ya kulala muda mrefu au muda mfupi. Ikiwa mtoto ananyonya, usimpe titibandia hadi awe amenyonya kikamilifu. Kunyonyesha kunahusishwa na kupungua kwa hatari ya SIDS.
  • Tumia godoro thabiti (lililofunikwa kwa shuka iliyokazwa) ili kuzuia nafasi baina ya godoro na pande za hori, yadi ya kucheza au tenga la mtoto. Hatua hii inaweza kupunguza hatari ya kunaswa, kukosa hewa na SIDS.
  • Usiweke mto, mablanketi mazito, au wanyama bandia kwenye hori. Vitu hivi vinaweza kumkosesha mtoto hewa.
  • Kumfunga mtoto (kumfunga mtoto kwa kukaza kwenye blanketi) kunaweza kusababisha mtoto wako kuwa na joto zaidi. Usiruhusu mtoto wako awe na joto kupita kiasi.
  • Usiweke watoto wachanga kwenye kochi au kiti cha mikono ili alale. Kulala kwenye kochi au kiti cha mikono humweka mtoto kwenye hatari zaidi ya kifo, ikiwemo SIDS.
  • Usitumie viti vya mtoto mchanga, viti vya gari na bembea za mtoto mchanga kwa kulala mara kwa mara na usingizi kidogo wa kila siku. Hatua hizi zinaweza kusababisha uzuiaji wa njia ya hewa au mtoto kukosa hewa.
  • Usishiriki kitanda (kulala pamoja) na mtoto wako. Si salama.
  • American Academy of Pediatrics (AAP) inapendekeza kuwa watoto wachanga walale kwenye chumba kimoja na wazazi wao, karibu na kitanda cha wazazi wao, lakini katika kitanda tofauti au hori bora kwa watoto wachanga. Mpango huu wa kulala unapendekezwa haswa kwa mwaka wa kwanza wa mtoto, lakini unapaswa kudumishwa angalau kwa miezi 6 ya kwanza.
  • Weka hori, matenga ya watoto na yadi za kucheza katika maeneo yasiyo na hatari—yale yasiyo na kamba, nyaya, au mapazia ya dirisha yanayoning`inia—ili kupunguza hali ya kujinyonga.
  • Usitumie monita za upumuaji wa moyo na vifaa vya biashara—kabari, vishikaji nafasi na magodoro maalum—ili kusaidia kupunguza hatari ya SIDS na vifo vya watoto wachanga vinavyohusiana na kulala. Vifaa hivi havijathibitisha kuzuia SIDS. Vimesababisha kifo cha mtoto mchanga kwa nadra sana.
  • Jadili masuala haya na mengine ya afya na usalama na mtoa huduma ya afya wa mtoto wako.

Vidokezo vya usalama

  • Ili kuzuia michomo, usibebe wala kunywea vioevu moto kama vile kahawa karibu na mtoto. Punguza halijoto ya kichemshio cha maji hadi 120°F (49°C) au chini.
  • Usivute wala kuruhusu wengine wavute sigara karibu na mtoto. Ikiwa wewe au wanafamilia wengine wanavuta sigara, vutia nje na si karibu na mtoto kamwe.
  • Kwa kawaida ni sawa kumpeleka mtoto nje. Lakini kaa mbali na maeneo yeliyobanana na kujaa watu ambapo viini vinaweza kusambaa. Unaweza kuwaalika wageni nyumbani mwako kumwona mtoto wako mradi tu wasiwe wagonjwa.
  • Unapompeleka mtoto nje, usikae muda mrefu sana kwenye mwangaza wa jua wa moja kwa moja. Mfunike mtoto au nenda kwenye kivuili.
  • Mweke mtoto kwenye kiti cha gari kinachoangalia nyuma ukiwa garini kila mara. Hii inapaswa kuwekwa kwenye kiti cha nyuma kulingana na maelekezo ya kiti cha gari. Usiwahi kumwacha mtoto wako peke yake garini.
  • Usimwache mtoto wako kwenye sehemu ya juu, kama vile meza, kitanda wala kochi. Anaweza kuanguka na kuumia.
  • Huenda ndugu wakubwa wakataka kumshika, kucheza naye na kutaka kumjua mtoto. Hii ni sawa mradi tu mtu mzima anaangalia.
  • Wasiliana na mtoa huduma wa afya mara moja ikiwa mtoto wako ana homa (tazama Homa na watoto, hapa chini)

Homa na watoto

Tumia kipimajoto cha dijitali kuangalia halijoto ya mtoto wako. Usitumie kipimajoto za zebaki. Kuna aina tofauti na matumizi ya vipimajoto vya dijitali. Vinajumuisha:

  • Rektamu. Kwa watoto walio chini ya miaka 3, halijoto ya rektamu ni sahihi zaidi.
  • Paji la uso (panja). Hii hufanya kazi kwa watoto walio na umri wa miezi 3 na zaidi. Ikiwa mtoto chini ya miezi 3 ana dalili za ugonjwa, hii inaweza kutumiwa kwa pasi ya kwanza. Mtoa huduma anaweza kutaka kuthibitisha kwa halijoto ya rektamu.
  • Sikio (kiwambo cha sikio). Halijoto za sikio ni sahihi baada ya umri wa miezi 6, lakini si kabla.
  • Kwapa (kwapajani). Hii ndiyo inayoaminika kidogo lakini inaweza kutumiwa kwa pasi ya kwanza kuangalia mtoto wa umri wowote aliye na ishara za ugonjwa. Mtoa huduma anaweza kutaka kuthibitisha kwa halijoto ya rektamu.
  • Mdomo. Usitumie kipimajoto ndani ya kinywa cha mtoto wako hadi awe na miaka 4.

Tumia kipimajoto cha rektamu kwa uangalifu. Fuata maelekezo ya mtengenezaji bidhaa kwa matumizi sahihi. Kiweke taratibu. Kiweke lebo na uhakikishe hakijatumiwa mdomoni. Huenda kikapita kwenye viini kutoka kwenye choo. Ikiwa unahisi si Sawa kutumia kipimajoto cha rektamu, mwulize mtoa huduma wa afya aina ya kutumia badala yake. Ukizungumza na mtoa huduma yeyote wa afya kuhusu homa ya mtoto wako, mwambie aina uliyotumia.

Hapa chini pana miongozo ya kujua ikiwa mtoto wako ana homa. Mtoa huduma wa afya wa mtoto wako anaweza kukupa nambari tofauti za mtoto wako. Fuata maagizo mahususi ya mtoa huduma wako.

Vipimo vya homa vya mtoto chini ya miezi 3:

  • Kwanza, mwulize mtoa huduma wa afya wa mtoto wako jinsi unavyopaswa kupima halijoto.
  • Rektamu au paji la uso: 100.4°F (38°C) au juu zaidi
  • Kwapa: 99°F (37.2°C) au juu zaidi

Vipimo vya homa vya mtoto wa miezi 3 hadi miezi 36 (miaka 3):

  • Rektamu, paji la uso, au sikio: 102°F (38.9°C) au juu zaidi
  • Kwapa: 101°F (38.3°C) au juu zaidi

Wasiliana na mtoa huduma wa afya katika hali hizi:

  • Halijoto ya kurudia ya 104°F (40°C) au juu zaidi kwa mtoto wa umri wowote
  • Homa ya 100.4° (38°C) au juu zaidi kwa mtoto chini ya miezi 3
  • Homa inayodumu zaidi ya saa 24 kwa mtoto chini ya miaka 2
  • Homa inayodumu kwa siku 3 kwa mtoto wa miaka 2 au zaidi

Chanjo

Kulingana na mapendekezo kutoka AAP, kwenye ziara hii mtoto wako anaweza kupata chanjo ya homa ya ini B ikiwa bado hakupata hospitalini.

Uchovu kwa mzazi: Tatizo la kuchosha

Kumtunza mtoto aliyezaliwa kunaweza kuchosha kimwili na kihisia. Sasa hivi inaweza kuonekana kuwa huna muda wa kitu kingine. Lakini kujitunza vizuri kutakusaidia kumtunza mtoto wako pia. Hivi hapa baadhi ya vidokezo:

  • Pumzika. Wakati mtoto wako analala, tenga muda wako binafsi. Lala usingizi kidogo au pumzika. Jua wakati wa kusema “huhitaji” wageni. Ikiwa hujapumzika, puuza mkusanyiko wa vitu nyumbani na usimamishe kazi ambazo si muhimu. Jipe muda wa kutosha ili uzoee jukumu jipya la kuwa mzazi.
  • Kila chakula kizuri. Lishe zuri linakupa nguvu. Na ikiwa umejifungua hivi punde, kula vizuri huusaidia mwili wako kupona. Jaribu kula matunda, mboga za majani, nafaka na protini mbalimbali. Epuka vyakula vya “kupika haraka”. Na upunguze kafeini haswa ikiwa unanyonyesha. Dumisha maji mwilini kwa kunywa maji ya kutosha.
  • Kubali usaidizi. Kumtunza mtoto aliyezaliwa kunaweza kukulemea. Usiogope kuomba usaidizi kutoka kwa watu wengine. Ruhusu familia na marafiki kusaidia kwa kazi za nyumbani, milo na kufua, ili wewe na mwenzako mpate muda wa kutangamana na mtoto wenu aliyezaliwa. Ikiwa unahitaji usaidizi zaidi, zungumza na mtoa huduma wa afya kuhusu machaguo mengine.

Uchunguzi unaofuata kwenye: _______________________________

MADOKEZO YA MZAZI:

Powered by
Disclaimer